Kutokana na ongezeko la mahitaji ya pesa kwa watu wengi na uhaba wa kipato katika kutimiza mahitaji hayo,watu wemgi tumejikuta tukishindwa katika kutimiza zile ndoto na matarajio yetu ambayo kimsingi yamekuwa na utegemezi mkubwa wa pesa. biashara,ujenzi.elimu na mahitaji mbalimbali ni moja ya vitu ambavyo vimekuwa ni changamoto kubwa sana katika kuvitimiza katika mazingira ya uhaba wa pesa tulioanao.
Kwa hali hii ndipo ambapo watu tumeamua kutafuta njia mbadala ya kuweza kupata pesa ambazo zitaweza kukidhi mahitaji hayo na kuweza kutimiza ndoto zetu,na njia kuu ambayo wengi wetu tumejiingiza na kutumia sana ni njia ya kupata pesa kwa njia ya MKOPO. njia ambayo imekuwa mkombozi mkubwa sana kwa watu wengi lakini pia imekuwa msumari wa moto kwa watu wengine,na hii yote ni kutokana na namna ya utafsiri wa mkopo wenyewe,njia za upatikaji wake na hata matumizi ya mkopo huo hadi kufikia suala la urejeshi wa mkopo huo.
Nini maana ya MKOPO??